Inaunda akaunti ya LG
Katika Usimamizi wa Akaunti, unaweza kutumia anwani yako ya barua pepe kuunda akaunti mpya ya LG.
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kithibiti cha mbali na uchague Aikoni ya MipangilioAikoni ya Mipangilio upande wa juu kulia.
  2. Chagua Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Jumla Usimamizi wa Akaunti.
  3. Chagua FUNGUA AKAUNTI. Soma na ukubaliane na Sheria za Huduma.
  4. Ingiza kitambulisho na nenosiri. Kitambulisho chako lazima kiwe anwani yako ya barua pepe.
  5. Ingiza tarehe yako ya kuzaliwa.
  6. Chagua SAWA. Enda kwenye barua pepe yako ili uthibitishe anwani yako ya barua pepe. Tafadhali thibitisha barua pepe yako kabla muda haujaisha.
  7. Ingia kwa kutumia akaunti yako mpya ili uanze kutumia huduma.
Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
Muunganisho wa Intaneti unahitajika kuunda akaunti.
Malezo yanayohitajika huenda yakatofautiana kutegemea nchi.
Vitambulisho vilivyopo na ambavyo havitumii anwani ya barua pepe vinaweza kubadilishwa kuwa anwani yako ya barua pepe.
Huenda ufikiaji wa huduma ukadhibitiwa kulingana na umri wako.
Ili kutatua tatizo linalihusiana na utendaji huu, rejelea sehemu ya Utatuzi ya Mwongozo wa Mtumiaji.