Kutumia Mobile Connection
Mobile Connection hukuruhusu kushiriki na kufurahia maudhui yaliyohifadhiwa kwenye vifaa mahiri vya watu kupitia televisheni yako.
Inapendekezwa kuwa vifaa vyako mahiri vya Android viendeshe Lollipop au matoleo ya baadaye ya Android.
Inaunganisha kifaa mahiri na Mobile Connection
Sanidi muunganisho kwa kufuata mwongozo ulio hapo chini:
  1. Sanikisha programu ya LG TV Plus kwenye kifaa mahiri.
  2. Unganisha nuninga yako na kifaa mahiri kwenye mtandao sawa wa Wi-Fi.
  3. Fungua programu ya LG TV Plus na usanidi muunganisho kwenye televisheni yako ukifuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye skrini.
  4. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO ili kuonyesha, na oroodha ya vifaa mahiri vilivyounganishwa vitaonekana upande wa kulia wa skrini.
  5. Chagua kifaa chako mahiri unachokipendelea.

Kifaa mahiri kilichounganishwaKifaa mahiri kilichounganishwa

Vifaa mahiri vya Android vitajaribu kuunganisha kiotomatiki vikiingia katika eneo lililo na mtandao baada ya muunganisho wa kwanza kupatikana.
Unashiriki maudhui na Mobile Connection
Unaweza kushiriki na kufurahia maudhui yaliyohifadhiwa kwenye kifaa chako mahiri kupitia televisheni yako.
  1. Fungua programu ya LG TV Plus iliyosakinishwa kwenye kifaa chako mahiri.
  2. Sanidi maudhui unayoyapendelea kwenye televisheni.
Vipengee vinavyotumika vinaweza kutofautiana kutegemea toleo na mtengenezaji wa mfumo wa kuendesha kifaa chako mahiri.