Kutumia Kidhibiti cha Skrini
Unaweza kudhibiti vifaa vya nje vilivyounganishwa na televisheni yako kwa kutumia Kidhibiti cha Skrini kilichoonyeshwa kwenye skrini ya televisheni yako.
-
Bonyeza kitufe cha
katika Kidhibiti Mbali Mahiri.
- Kutumia Kidhibiti Mbali Mahiri, cahgua kitufe unachopendelea kwenye Kidhibiti cha Skrini kilichoonyeshwa katika skrini ya televisheni yako.
-
Sanidi Anzisha Vidhibiti Kamili kwa vifaa vya nje vilivyounganishwa na televisheni yako.
Unapochagua kifaa, Kidhibiti cha Skrini hubadilika na kuwa kidhibiti cha mbali cha kifaa chako.
Ikiwa upau wa sauti umeunganishwa, Kidhibiti cha mbali cha Skrini kinaweza kutumiwa kama kidhibiti cha mbali cha upau wa sauti.Kwa maelezo zaidi, angalia Jinsi ya Kuendesha TV Kidhibiti Mbali cha Jumla katika Mwongozo wa Mtumiaji. -
Maelezo mbalimbali yanayohusiana na kipindi unachotazama yataonekana katika sehemu ya chini ya skrini.
Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.Ili kuona maelezo, bofya Furahia Vipindi vya TV vya Moja kwa Moja KIUNGO MAGIC katika Mwongozo wa Mtumiaji.
-
Unaweza kupiga picha skrini ya televisheni yako.
Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli pekee.Unaweza kutazama / kufuta picha zilizopigwa kwenye skrini katika programu ya Picha & Video.Unaweza kunakili picha zilizopigwa kwenye skrini uzibandike kwenye kifaa cha hifadhi cha USB katika programu ya Picha & Video.
(Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.) -
Unaweza kukuza ndani hadi kwa sehemu fulani za skrini kwa kutumia Focus Zoom.
Kwa maelezo zaidi, angalia Manufaa ya TV Inayoweza Kuunganishwa kwenye Intaneti Kupanua Sehemu ya Picha Unayotaka katika Mwongozo wa Mtumiaji.
- Vitufe vinavyofaa kwa kifaa kilichochaguliwa vitatokea.
- Utaona vitufe zaidi vya kidhibiti cha mbali.
- Unaweza kuanzisha programu ya KIUNGANISHI CHA KIFAA. Unaweza kuweka kiungambali kinachotumika katika vifaa mbalimbali.
- Unaweza kubadilisha mkao wa kidhibiti cha Mbali cha Skrini.
Kipengee hiki kinaweza kutumiwa tu na Kidhibiti Mbali Mahiri.
Unaweza kununua Kidhibiti Mbali Mahiri kando ikiwa haikujumuishwa.
Aina ya vitufe vinavyotokea kwenye Skrini ya Kidhibiti hutofautiana, kulingana na eneo na aina ya kifaa kilichounganishwa.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli na nchi.