Kutumia Sauti kuwa Matini
Unaweza kuandika matini katika sehemu za matini kwa kutumia kipengele cha kutambua sauti.
Chagua kitufe cha
kwenye skrini ya kibodi ili ubadilishe uanze kutumia hali ya kuingiza usemi.
Chagua kitufe cha
kwenye skrini ya kibodi ili ubadilishe uanze kutumia hali ya kuingiza usemi.
Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli au katika baadhi ya nchi pekee.
-
Sogeza kiashiria cha Kidhibiti Mbali Mahiri katika kisanduku cha kuweka maandishi ili ufungue kibodi pepe.
-
Bofya kitufe cha
kwenye kibodi pepe.
-
Baada ya kidirisha cha kutambua sauti kufunguka inavyoonyeshwa hapa chini, zungumza polepole na kwa utaratibu kwenye maikrofoni ya kidhibiti cha mbali.
-
Ikiwa kuna maneno yanayofanana na uliyotamka kwa sauti, huenda uone orodha ya matokeo kadhaa kama ilivyoonyeshwa hapana chini.
Usipopata matokeo unayotaka, bonyeza JARIBU UPYA ujaribu tena.
Chagua matokeo na yataonyeshwa kwenye kisanduku cha matini.
Tahadhari unapotumia Sauti kuwa Matini
Angalia muunganisho wa mtandao kabla ya kutumia Sauti kuwa Matini.
Unaweza kubadilisha huduma ya utambuzi wa sauti katika
Jumla Lugha (Language) Lugha ya Utambuzi wa Sauti.
Ili kubadilisha kwa muda mfupi hadi lugha nyingine ya utambuzi wa sauti, bonyeza kitufe cha
kilicho katika dirisha la kuonyesha utambuzi wa sauti.
Jumla Lugha (Language) Lugha ya Utambuzi wa Sauti.
Ili kubadilisha kwa muda mfupi hadi lugha nyingine ya utambuzi wa sauti, bonyeza kitufe cha
kilicho katika dirisha la kuonyesha utambuzi wa sauti.
Unaweza kutumia utendaji huu tu baada ya kukubaliana na sheria za Utambuzi wa Sauti.
Gharama ya Sauti kuwa Matini inaweza kutofautiana kutegemea sifa za mtumiaji (sauti, matamshi, kiimbo,na kasi ya kusema) na mazingira (kelele na ukubwa wa sauti ya televisheni).
Ili kuboresha usahihi wa Sauti kuwa Matini, lazima uzungumze kwa uwazi na kwa sauti ukiwa takribani centimita 10 (inchi 4) kutoka kwenya maikrofoni ya Kidhibiti Mbali Mahiri.
Huduma ya utambuzi wa sauti haipatikani katika sehemu yoyote inayohitaji uingize nywila na upau wa kuweka anwani ya Kivinjari cha Tovuti yako (haijumuishi utafutaji wa kawaida).