Kutumia puku cha USB Kinachotumia Nyaya / Isiyotumia Nyaya
Unganisha puku chako kwenye shimo la USB. Tumia puku kuashiria skrini ya televisheni na uchague menyu unayoitaka.
Kitufe cha upande wa kulia na vitufe maalum vilivyo kwenye puku havifanyi kazi.
Unapotumia puku / kibodi ya USB ya pasi waya, matumizi yanaweza kuathiriwa na umbali na hali ya kifaa chenyewe.
Kutumia Kibodi ya USB Inayotumia Nyaya / Isiyotumia Nyaya
Unganisha kibodi yako kwenye shimo la USB. Unaweza kuingiza maandishi kwa kutumia kifaa cha kibodi kilichounganishwa.
Haiwezekani kuingiza maandishi katika baadhi ya skrini.
Inapendekezwa kwamba utumie bidhaa ambazo zimefanyiwa majaribio na kuonekana kwamba zinaingiliana na televisheni za LG.
LOGITECH K360, LOGITECH K400, LOGITECH K750, LG Electronics MKS-1200
Unaweza kubadilisha lugha kwa kubonyeza kibonye cha kubadilisha lugha au kibonye cha Alt kilicho kulia. Pia unaweza kubadilisha kwa kubonyeza kibonye cha Ctrl na kibonye cha nafasi wakati mmoja.
Matumizi ya kibodi ya USBya pasi waya yanaweza kuathiriwa na umbali wa kifaa au mazingira kilipo kifaa.
Ili kuingiza maandishi katika sehemu ya kuweka maandishi, tumia kibodi ya kwenye-skrini au kibodi ya USB.