Kutumia Utendaji wa TV kupitia kipengele cha Kutamka
Unaweza kufikia vipengele vya utendaji vya TV kwa urahisi na hara kupitia kipengele cha utambuzi wa usemi.
-
Bonyeza na ushikilie kitufe cha
kwenye kidhibiti mbali utamke utendaji unaotaka kuanzisha au neno muhimu unalotaka kutumia kwa utafutaji wako.
-
Ukiachilia kitufe cha
baada ya kuingiza usemi wako, utendaji unaolingana utaanzishwa.
Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli au katika baadhi ya nchi pekee.
Ili utumie utendaji huu vizuri, Lugha ya Utambuzi wa Sauti na Lugha ya Menyu sharti ziwekwe kwenye lugha moja.
Ni lazima Eneo yako ilingane na lugha ya matokeo halisi ya utafutaji.
Baadhi ya vipengee huenda visipatikane ikiwa mipangilio ya eneo na ya lugha yako ni tofauti.
Unaweza kubadilisha huduma ya utambuzi wa sauti katika
Jumla Lugha (Language) Lugha ya Utambuzi wa Sauti.
Jumla Lugha (Language) Lugha ya Utambuzi wa Sauti.
Maelezo ya huduma yanaweza kutofautiana kulingana na nchi.
Tafadhali fahamu kuwa Huduma ya AI inaweza kubadilishwa, kuondolewa au kusimamishwa bila ilani na LGE au watoa huduma wake wengine.
Bonyeza kitufe cha
kwenye kidhibiti mbali ili utazame mifano ya utendaji unaoweza kutumia kwa kipengele cha kudhibiti kwa kutamka.
kwenye kidhibiti mbali ili utazame mifano ya utendaji unaoweza kutumia kwa kipengele cha kudhibiti kwa kutamka.
Vipengee vinavyopatikana
Tumia vipengele vyaa TV
- Unatazama TV
- Zima TV / Punguza/ongeza Sauti / Idhaa juu/chini / Idhaa 20 (nambari ya idhaa) / Idhaa OOO (jina la idhaa) / Cheza 'OOO(jina la kipindi)' / Nionyeshe wakati 'OOO(jina la kipindi)' kinapoanza / Rekodi 'OOO(jina la kipindi)' / Washa Live Playback
- Badilisha maingizo
- Nionyeshe orodha ya maingizo / HDMI 1 / Anza kutumia kiweko cha mchezo / Anza kutumia king`amuzi
- Badilisha mipangilio
- Angaza/fifisha skrini / Weka skrini iwe dhahiri zaidi / Modi ya Picha ya Sinema (chaguo la modi ya picha) / 16:9 Aspect Ratio (chaguo la aspect ratio) / Modi ya Sauti Wastani (chaguo la modi ya sauti) / Badilisha hadi Modi ya Mchezo / Unganisha Bluetooth / Badilisha hadi HDMI ARC (chaguo la Zao la Sauti)) / Zima TV baada ya dakika 30 / Washa Maelezo ya Video / Washa Mwongozo wa Sauti / Washa Manukuu Yaliyofungwa
- Nenda kwenye vipengele/programu
- Nyumbani / Za hivi karibuni / UFIKIAJI WA HARAKA / Mipangilio / Mipangilio ya picha / Mipangilio ya sauti / Mipangilio ya idhaa / Mipangilio ya mtandao
Tafuta kutoka kwenye TV
- Tafuta vipindi vya TV na VOD
- Tafuta 'OOO(jina la kipindi)' / Tafuta vipindi vya TV vinavyomhusisha 'OOO(jina)' / Nionyeshe filamu / Nionyeshe vipindi vya TV vinavyoanza saa 7 jioni / Nipendekezee kitu cha kutazama
- Tafuta taarifa zaidi kuhusu maudhui
- Nitafutie nyimbo za 'OOO(jina la kipindi)' / Ni nani mwelekezi wa 'OOO(jina la filamu)'? / Nionyeshe ploti ya 'OOO(jina la kipindi)'
- Tafuta maudhui yangu
- Nionyeshe picha zangu / Cheza muziki wangu / Cheza rekodi ya 'OOO(jina la kipindi)'
- Tafuta taarifa nyingine
- 'OOO(jina)' ni nani? / Hali ya hewa iko vipi leo? / Ni saa ngapi sasa 'OOO(jina la eneo)'?
- Tafuta kwenye Mwongozo wa Mtumiaji
- Nitafutie 'OOO(jina la kipengele)' kutoka kwenye Mwongozo wa Mtumiaji
Tahadhali za Utambuzi wa Sauti
Utambuzi wa sauti huhitaji Kidhibiti Mbali Mahiri, ambayo huenda hatumiki katika baadhi ya modeli.
Ili kutumia vipengee vyote vya kutambua sauti, unahitajika kuweka mtandao wako, vituo, eneo n.k. La sivyo, huwezi kutumia baadhi ya vipengee.
Ikiwa hujaunganisha kwenye mtandao, huenda usiweze kutumia vipengele fulani vya autendaji kwa kutumia majina ya idhaa.
Kama una muunganisho wa mtandao, unahitajika kukubaliana na sheria na masharti ili kutumia huduma ya kutambua sauti.
Ili kudhibiti king`amuzi kilichounganishwa kwenye TV kwa kipengele cha kutambua sauti, nenda kwenye
KIUNGANISHI CHA KIFAA ili uweke Universal Control.
KIUNGANISHI CHA KIFAA ili uweke Universal Control.
Inapendekezwa kuelekeza Magic Remote upande wa king’amuzi baada ya ingizo la sauti.
Kiwango cha utambuzi wa sauti kinaweza kutofautiana kutegemea sifa za mtumiaji (ukubwa wa sauti, matamshi, lafudhi na kasi ya kuzungumza) na mazingira (kelele na ukubwa wa sauti ya TV).
Ili kutambua sauti yako kwa njia sahihi, lazima utamke maneno taratibu na kwa njia sahihi ukitumia ukubwa wa sauti unaofaa kwa umbali wa sentimita 10 hivi (Inchi 4) kutoka kwa maikrofoni ya Kidhibiti Mbali Mahiri.
Kama sauti yako haitatambuliwa vyema, huduma ya utambuzi wa sauti inaweza kufanya kazi kwa njia tofauti na jinsi ulivyonuia.