Kutumia Menyu ya Moja kwa Moja
Unaweza kutumia vipengele vinavyohitajika kwa urahisi unapotazama matangazo ya TV.
-
Endesha Live TV kwa kubonyeza
.
-
Sogeza kielekezi cha Kidhibiti Mbali Mahiri upande wa kulia wa skrini ya TV. Pia unaweza kubonyeza kitufe cha kwenye Kidhibiti chako cha Mbali ili uone Menyu ya Moja kwa Moja.
Unaweza kuionyesha kwa kubonyeza kitufe cha au kitufe cha kwenye kidhibit mbali hata wakati hutazami kipindi chochote.
-
Idhaa
:
Angalia orodha ya maudhui ambayo yanatangazwa kwa sasa.
Chagua Idhaa tena huku orodha ikiwa imefunguka ili utazame Mwongozo wa TV.
Rejelea Furahia Vipindi vya TV vya Moja kwa Moja Mwongozo wa TV katika Mwongozo wa Mtumiaji upate maelezo kwenye Mwongozo wa TV. - Inapendekezwa : Pata mapendekezo ya vituo na programu kulingana na historia yako ya utazamaji.
Vituo vilivyoonyeshwa kwenye Orodha ya Vituo ni jumla ya vituo vinavyotolewa na mtoa huduma za matangazo. Kwa hivyo, ikiwa mtoa huduma za matangazo amebadilisha usanidi wake bila kutoa ilani, vituo vitakavyoonekana kwenye Orodha ya Vituo vinaweza kuwa tofauti na vituo halisi vya TV.
Kwa kuwa maelezo ya kituo yanayoonekana kwenye Orodha ya Vituo yanajumuisha maelezo yaliyotolewa na watoa huduma wa nje wa Mwongozo wa Kielektroniki wa Vipindi (EPG), inaweza kuwa tofauti na vituo halisi vya TV.
Ili kupokea huduma za kupendekeza zinazofaa, unahitaji kuweka mipangilio ya mtandao wako, eneo na urekebishaji wa kiotomatiki.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea nchi.