Kuweka mipangilio ya vituo kiotomatiki
MWANZOMWANZO Aikoni ya MipangilioAikoni ya Mipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Idhaa Kitiuni Idhaa & Mipangilio Kutuuni Kioto
Hutuni vituo kiotomatiki.
  1. Chagua Nchi ambamo TV itatumika. Mipangilio ya Vituo hubadilika kulingana na nchi uliyochagua.
  2. Anzisha Kutuuni Kioto.
  3. Chagua modi za kutuni vituo.
  4. Weka kutuni kiotomatiki unaofuata maelekezo kwenye skrini.
Kama Chanzo cha Ingizo hakijaunganishwa ipasavyo, huenda usajili wa kituo usifaulu.
Kutuuni Kioto hupata tu vituo ambavyo vinatangaza kwa sasa.
Ikiwa Usalama imewashwa, kidirisha ibukizi kitajitokeza kikiuliza nenosiri.
Weka mipangilio ya Kebo
Unapotafuta vituo ukitumia mipangilio KAMILI, inaweza kuchukua muda.
Thamani zifuatazo zinahitajika ili kutafuta vituo vyote vinavyopatikana kwa haraka na usahihi. Thamani zinazotumiwa sana zimewekwa kama chaguo msingi.
Vipengee vinavyoweza kusanidiwa kulingana na Aina.
Masafa (kHz)
Weka marudio yanayolingana na mapendeleo ya mtumiaji.
Kiwango cha Ishara (kS/s)
Kasi ya kifaa kama vile modemu ya kutuma ishara kwenye kituo.
Ubadilikaji
Kupakia ishara za sauti au video kwa mtoa huduma.
Kitambulisho cha Mtandao
Kitambulisho cha kipekee kilichotengwa kwa kila mtumiaji.
Anza Masafa(kHz)
Weka masafa ya marudio ya kuanza yanayolingana na mapendeleo ya mtumiaji.
Kamilisha Masafa(kHz)
Weka masafa ya marudio ya kumaliza yanayolingana na mapendeleo ya mtumiaji.
Weka mipangilio ya setilaiti
Unaeza kuongeza / kufuta / kuweka setilaiti unayotaka.
Ikiwa mipangilio ya vituo imewekwa kuwa Setilaiti
Setilaiti
Chagua Setilaiti unayotaka.
Masafa ya LNB
Chagua kiwango kimoja kati ya 9750/10600, 9750/10750, 9750, 10600, 10750, 11300, 5150, MDU1, MDU2, MDU3, MDU4, MDU5. Ukichagua 9750/10600, 9750/10750(MHz), Toni 22kHz itazimwa. Ikiwa huwezi kupata kiwango cha marudio ya LNB kutoka kwenye orodha, chagua Mtumiaji na uweke marudio.
Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
Kipokea Ishara
Chagua transponda unayotaka kuweka.
Toni 22kHz
Unapotumia swichi ya toni ya 22kHz, chagua 22kHz au 0 Hz. Ukitumia Toni 22kHz, Kebo moja na aina ya Mota zitazimwa.
Nguvu za LNB
Ili kuwasha umeme wa LNB, chagua Imewashwa. Ukichagua Imezimwa, Aina ya Mota itazimwa.
DiSEqC
Unapotumia DiSEqC, teua chaguo moja kati ya A~D na ToniA~B. Ukitumia DiSEqC, Kebo moja na aina ya Mota zitazimwa.
Unicable
Chagua Washa ili utumie kipengele cha Kebo Moja na uweke mipangilio ya Kebo moja kwenye menyu ya Mipangilio ya unicable. Wakati kipengele cha Kebo Moja kimewashwa, Toni 22kHz, DiSEqC, Aina ya Mota itazimwa.
Kipengele hiki utaonyeshwa kama SatCR katika baadhi ya aina.
Aina ya Mota
Chagua Aina ya Mota ili utumie Mota na uweke Mota hiyo katika menyu ya Mipangilio ya Mota. Mota ikiwashwa Toni 22kHz, DiSEqC, Unicable itazimwa.
Ukiweka mipangilio ya setilaiti kwa zingine, lazima uongeze kifaa cha ishara ukitumia kipengele cha Ubadilishaji wa kifaa cha ishara.
Unapochagua Toni ya 22kHz Tone na DiSEqC, lazima uziunganishe katika sehemu sawa na ile iliyooneshwa kwenye OSD.
Ukifuta Setilaiti, vituo vyote vilivyohifadhiwa kwenye Setilaiti hiyo vitafutwa.
Weka Mipangilio ya Mota
DiSEqC 1.2 : Dhibitii mota ili kubadilisha mahali dishi ya setilaiti ilipo.
Mwelekeo wa Kuendesha
Chagua upande unaotaka kuelekeza mota.
Modi ya Kuendesha
Modi mbili zinapatikana: Ya hatua na Inayoendelea.
  • Hatua : Mota husonga kulingana na thamani uliyoweka (kutoka 1 hadi 128).
  • Inayoendelea : Mota inasonga bila kusimama hadi utakapobonyeza Simama.
Jaribu Kipokea Ishara
Chagua Transponda ya jaribio unalotaka kuweka.
Weka upeo
Weka mwenendo wa mota kuelekea mashariki au magharibi ili isonge kulingana na maelekezo yaliyowekwa.
  • Imewashwa : Unaweza kudhibiti usambazaji kuelekea upande wa sasa kwa kuchagua Magharibi / Mashariki.
  • Imezimwa : Unaweza kughairi kiwango cha mwisho ulichoweka.
NENDA KWA 0
Unaweza kubadilisha mota iwe sufuri.
USALS : Weka mahali ulipo sasa (Longitudo / Latitudo).