Kutumia Kipengele cha Wi-Fi Direct
Mtandao
Wi-Fi Direct
Wi-Fi Direct ni kipengele aambacho kinawezesha runinga yako kijiunge na vifaa vinavyoweza kutumia Wi-Fi Direct bila kutumia Kisambaza Data Kisichotumia Waya. Unaweza kufungua faili zilizohifadhiwa kwenye vifaa vilivyounganishwa ukitumia Wi-Fi Direct katika programu ya Picha & Video na programu ya Muziki app.
- Washa Wi-Fi Direct kwenye kifaa ambacho ungependa kuunganisha.
- Kwenye orodha ya vifaa vinavyoweza kuunganishwa, chagua TV itakayounganishwa.
- Baada ya kukubali ombi la kuunganisha kwenye TV, Wi-Fi Direct itaunganishwa.
- Kutoka katika kifaa unachotaka kuunganisha, chagua video, muziki au picha unayotaka kufungua kwenye runinga yako ukitumia kipengee cha kushiriki kwenye kifaa chako.
- Unaweza kufungua faili zilizohifadhiwa kwenye vifaa vilivyounganishwa ukitumia Wi-Fi Direct katika programu ya Picha & Video na programu ya Muziki app.
Ikiwa kifaa kilichounganishwa awali kwenye TV kitatuma tena ombi la kuunganisha, kitaunganishwa kiotomatiki.
Ukianzisha programu ya Screen Share wakati Wi-Fi Direct imeunganishwa, Wi-Fi Direct itatenganishwa.