Kuweka Chaguo za Kina za Mipangilio ya Udhibiti
MWANZOMWANZO Aikoni ya MipangilioAikoni ya Mipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Picha Mipangilio ya Modi ya Picha Vithibiti vya Hali ya juu / Vidhibiti vya Kitaalamu
Ulinganuzi wenye Nguvu
Husahihisha tofauti iliyopo kati ya sehemu zenye mwangaza na zisizo na mwanga kwenye skrini ili kuboresha taswira kulingana na ung’aavu wa picha.
Dynamic Tone Mapping
Boresha mipangilio ya usawazishaji kulingana na mwanga wa picha wa maudhui ya HDR.
Rangi Inayobadilika
Ili kufanya picha iwe maridadi zaidi na kuvutia, rekebisha Rangi na usharabu wa picha.
Rangi Inayopendelewa
Hurekebisha rangi za ngozi, nyasi na mbingu ili iwe unavyopendelea.
Mwonekano Mzuri Kabisa
Hurekebisha mwonekano ili kufanya picha zilizofifia na zenye ukungu kung’aa.
Gama
Hurekebisha ung’aavu wa katikati katika picha.
Upeo wa Rangi
Huchagua safu za Rangi za kuonyesha. Weka upeo wa rangi kuwa Oto kulingana na mawimbi, au upate rangi bora zaidi kwa mpangilio wa Iliyopanuliwa na Pana.
Kichujio cha Rangi
Huchuja upinde wa jua mahsusi wa Rangi katika Rangi za Msingi ya RGB ili kupima na kusawazisha mwonekano wa rangi halisi.
Urari wa Weupe
Hurekebisha toni kwa jumla wa rangi kwenye skrini kuwa unavyotaka.
Mfumo wa Usimamizi wa Rangi
Hiki ni kipengele ambacho hutumiwa na wataalamu wanaporekebisha Rangi kwa kutegemea ruwaza ya majaribio ya Rangi sita (Nyekundu / Kijani / Bluu / Sayani / Majenta / Njano) bila kuathiri sehemu zingine za Rangi.
Kwa picha za kawaida, urekebishaji unaweza kosa kusababisha mabadiliko yanayoweza kutambulika katika Rangi.
Chaguo zilizopo zinaweza kuwa tofauti kutegemea chanzo cha mawimbi au hali ya picha iliyochaguliwa.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.