Kusawazisha Hali ya Picha
Picha
Mipangilio ya Modi ya Picha
Kipengele hiki kinakuruhusu ubadilishe kwa kina hali uliyochagua ya picha.
- Mwanga Nyuma
-
Hudhibiti kiasi cha ung’aavu wa skrini na kurekebisha mwanga wa skrini. Kadri inayokaribia 100 ndivyo inavyong’aaa zaidi.
Punguza Mwanga Nyuma ili upunguze matumizi ya umeme.Kutegemea Kuhifadhi Nishati (Oto / Kiwango cha juu), huenda hutaweza kubadilisha Mwanga Nyuma.
Katika hali hii, nenda kwenye
Picha Kuhifadhi Nishati kisha uweke Imezimwa au Kiwango cha chini.
- OLED LIGHT
- Hurekebisha ung’aavu wa skrini kwa kubadilisha ung’aavu katika paneli ya OLED.
- Ulinganuzi
- Hurekebisha utofautishaji wa rangi katika sehemu zenye ung’aavu na zenye giza kwenye picha. Ikiwa karibu na 100, utofautishaji huwa wa juu zaidi.
- Ung’aavu
- Hurekebisha ung’aavu wa jumla wa skrini. Ikiwa karibu na 100, ung’aavu utakuwa juu zaidi.
- Ukali
- Hurekebisha umadhubuti wa picha. Kadri ilivyo karibu na 50, ndivyo picha inavyokuwa madhubuti na kuonekana vizuri.
- Rangi
- Hupunguza au kuongeza kukolea kwa rangi kwenye skrini. Kadri ilivyo karibu na 100 ndivyo inavyokolea.
- Kivuli cha Rangi
- Hurekebisha usawa kati ya rangi nyekundu na kijani inayoonyeshwa kwenye skrini. Ikiwa karibu na Nyekundu 50, rangi itakuwa nyekundu zaidi. Ikiwa karibu na Kijani 50, rangi itakuwa kijani zaidi.
- Halijoto ya Rangi
- Hurekebisha hali joto ya rangi kutoka baridi kuwa vuguvugu.
Mipangilio unayoweka itatumika katika mbinu ya sasa ya kuingiza maudhui pekee.
Ili uweze kutumia mipangilio ya sasa ya picha kwenye mbinu zote za kuingiza maudhui, teua Tumia kwa maingizo yote.
Ili uweze kutumia mipangilio ya sasa ya picha kwenye mbinu zote za kuingiza maudhui, teua Tumia kwa maingizo yote.
Chaguo zilizopo zinaweza kuwa tofauti kutegemea chanzo cha mawimbi au hali ya picha iliyochaguliwa.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.
Kubadilisha Hali ya Picha
Picha
Mipangilio ya Modi ya Picha
Weka upya
Chaguo hili litabadilisha mipangilio ya Picha.
Unaweza kubadilisha hali za Picha tofautitofauti kwa kuchagua hali ya Picha unayotaka kubadilisha halafu uiwashe.