Kuchagua Hali ya Picha
MWANZOMWANZO Aikoni ya MipangilioAikoni ya Mipangilio Aikoni ya Mipangilio yoteAikoni ya Mipangilio yote Picha Mipangilio ya Modi ya Picha Modi ya Picha
Chagua hali ya picha inayofaa zaidi mazingira unapotazamia, mapendeleo yako au aina ya video.
Unapotumia mawimbi ya kawaida
Dhahiri
Huboresha picha kwa kuongeza utofautishaji, ung’aavu na umadhubuti.
Kawaida
Huonyesha picha zikiwa na viwango vya kawaida vya utofautishaji, ung’aavu na umadhubuti.
Eco / APS
Kipengele cha Kikokoa Umeme hubadilisha mipangilio ya runinga ili kupunguza matumizi ya umeme.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli na nchi.
Sinema
Skrini imeboreshwa ili kufaa utazamaji wa filamu.
Spoti / Soka / Kriketi
Skrini imeboreshwa ili kufaa utazamaji wa michezo. Huboresha umadhubuti wa picha zinazossogea kw akasi kama vile kupiga au kurusha mpira.
Jina la mchezo linaweza kuwa tofauti kutegemea nchi.
Mchezo
Skrini imeboreshwa ili kufaa uchezaji wa michezo ya video.
Athari ya HDR
Kipengele hiki hukuwezesha ufurahie picha iliyo safi zaidi inayobadilika vizuri kwa kurekebisha sehemu zilizo na mwanga mwingi za zile za mwanga chache kwenye picha.
Kipengele hiki hukupa picha inayokaribiana na uhalisi hata wakati usawa wa picha si mzuri.
Ukiweka Modi ya Picha kuwa Athari ya HDR, hutaweza kutumia baadhi ya Mipangilio ya Modi ya Picha.
Nembo ya TechnicolorNembo ya Technicolor Mtaalamu
Rangi hurekebishwa na wataalam mashuhuri Technicolor, wanaoshughulikia maudhui ya hali ya juu ya filamu za Hollywood.
Nembo ya isfNembo ya isf Mtaalam (Chumba Kiangavu) / Nembo ya isfNembo ya isf Mtaalam (Chumba cha Giza)
Humruhusu mtaalamu, au mtu mwingine yeyote anayejali ubora wapicha kusawazisha ili kupata picha bora zaidi. Chaguo hili ni menyu ya kubadilisha inayotolewa ili kutumiwa na wataalam wa kupata ubora wa picha waliofuzu mafunzo ya ISF. (Nembo ya ISF linaweza tu kutumiwa katika runinga zilizoidhinishwa na ISF.)
ISFccc : Imaging Science Foundation Certified Calibration Control.
Unapotumia mawimbi ya HDR / Advanced HDR / Dolby Vision
Dhahiri
Huboresha picha kwa kuongeza utofautishaji, ung’aavu na umadhubuti.
Kawaida
Katika mazingira ya kawaida ya kutazama, itafungua skrini inayoweza kuonyesha ubora na ung’aavu wa HDR.
Nyumba ya Sinema
Skrini huonekana ikiwa na mwanga na ung’aavu zaidi kushinda skrini ya Sinema.
Sinema
Skrini imeboreshwa ili kutumia mawimbi ya video ya HDR.
Mchezo
Skrini imeboreshwa ili kufaa uchezaji wa michezo ya video.
Nembo ya TechnicolorNembo ya Technicolor Mtaalamu
Rangi hurekebishwa na wataalam mashuhuri Technicolor, wanaoshughulikia maudhui ya hali ya juu ya filamu za Hollywood.
Video ya ubora wa HDR / Advanced HDR / Dolby Vision ikiwekwa katika runinga ambazo haziwezi kutumia teknolojia ya HDR / Advanced HDR / Dolby Vision, mitindo ya picha ya kawaida hutumiwa.
Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli na nchi.
Hali za picha zinaweza kuwa tofauti kutegemea mawimbi ya maudhui.
Wakati unapotazama maudhui ya mtandaoni, Hali ya Picha inaweza kubadilishwa ili kulingana na maudhui yanayoonyeshwa.
Nembo ya isfNembo ya isf Mtaalamu ni chaguo linalomruhusu mtaalamu wa ubora wa picha kuboresha mwonekano wa picha inayotimiza viwango. Kwa hivyo, huenda isifae kwa picha za kawaida.
Mabadiliko ya Modi ya Picha yanaweza kubadilisha Kuhifadhi Nishati na mipangilio ya Utunzaji wa Utumiaji wa Macho na yanaweza kuathiri matumizi ya nishati. Unaweza kubadilisha mipangilio mwenyewe kwenye menyu ya Kuhifadhi Nishati na Machaguo ya Picha.