Kucheza Muziki
Unaweza kusikiliza muziki kwa kutumia programu ya Muziki.
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kidhibiti cha mbali.
  2. Endesha programu ya Muziki.
  3. Chagua kifaa chako cha hifadhi unachokipendelea.
    Unaweza kuchagua nyimbo unazozipendelea kutoka kwa vifaa vyako vyote vya hifadhi na uziongeze kwa Orodha Chezeshi yangu.
  4. Chagua muziki unaoupenda na ufurahie.

Kicheza MuzikiKicheza Muziki

  1. Chagua orodha ya aina za maudhui unazozipendelea.
  2. Chagua na ufute maudhui unayoyataka.
    Unaweza kufuta faili ambazo zimeshirikiwa kutoka vifaa vingine.
  3. Chagua maudhui na uyaongeze kwa Orodha Chezeshi yangu.
  4. Unaweza kunakili maudhui na kuyabandika kwenye kifaa cha hifadhi cha USB.
    Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
  5. Washa kifaa cha kucheza muziki.
  6. Fungua Tafutiza.
Kutumia Chombo cha Kucheza Muziki
Chombo cha kucheza muziki hukuruhusu kuchagua muziki kutoka kwenye programu nyingine na kuutumia kama muziki wa mandharinyuma.
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kidhibiti cha mbali.
  2. Chagua Aikoni ya Kicheza Muziki cha JuuAikoni ya Kicheza Muziki cha Juu kwenye skrini ya televisheni yako.

Kicheza MuzikiKicheza Muziki

  1. Unaweza kucheza muziki kutoka kwa kifaa cha hifadhi kilichochaguliwa.
  2. Unaweza kuweka utendaji wa rudia muziki na cheza kutoka mahali fulani fulani.
  3. Vipengee vya kusanidiwa hutofautiana kutegemea modeli.
    Hali ya SkriniHali ya Skrini : Unaweza kuzima skrini unaposikiliza muziki au uoneshe chombo cha kucheza muziki katika hali ya skrini kamili.
    Skrini ImezimwaSkrini Imezimwa : Unaweza kusikiliza muziki skrini ikiwa imezimwa.
  4. Unaweza kubadilisha mahali kilipokaa chombo cha kucheza muziki.
  5. Unaweza kupunguza kicheza muziki.
  6. Kipengee hiki huzima chombo cha kucheza muziki.
  7. Muziki unapatikana kwa faili zinazoutoa.
    Katika baadhi ya faili za muziki, unawez kuchagua sehemu ya wimbo mahususi na usogeze mahali pa urudiaji.
    Kipengee cha nyimbo kinatumika tu kwenye baadhi ya vifaa.
    Maneno ya wimbo huenda hayataonekana kwa usawa kutegemea data ya maneno ya muziki yaliyo kwenye faili ya muziki.
Washa upya kifaa chako cha kucheza muziki kwa kubonyeza kitufe cha VOLUME kwenye kidhibiti chako cha mbali.
Huenda usiweze kutumia kicheza muziki kwa baadhi ya vipengee.
Umbizo la Sauti
Umbizo la Sauti
Umbizo la Faili Kipengele Maelezo
mp3 Kiwango cha Bit 32 kbps ~ 320 kbps
Kielelezo cha masafa 16 kHz ~ 48 kHz
Usaidizi MPEG-1, MPEG-2
Vituo mono, stereo
wav Kiwango cha Bit -
Kielelezo cha masafa 8 kHz ~ 96 kHz
Usaidizi PCM
Vituo mono, stereo
ogg Kiwango cha Bit 64 kbps ~ 320 kbps
Kielelezo cha masafa 8 kHz ~ 48 kHz
Usaidizi Vorbis
Vituo mono, stereo
wma Kiwango cha Bit 128 kbps ~ 320 kbps
Kielelezo cha masafa 8 kHz ~ 48 kHz
Usaidizi WMA
Vituo hadi vituo 6
flac Kiwango cha Bit -
Kielelezo cha masafa 8 kHz ~ 96 kHz
Usaidizi FLAC
Vituo mono, stereo
Idadi ya vituo vya muziki vinavyotumika vinaweza kutofautina kutegemea kielelezo cha masafa.