Kutazama Picha na Video
Unaweza kutazama picha na video ukitumia programu ya Picha & Video.
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kidhibiti cha mbali.
  2. Endesha Picha & Video programu ya.
  3. Chagua kifaa chako cha hifadhi unachokipendelea.
  4. Chagua na utazame picha au video unayopendelea.

Picha na VideoPicha na Video

  1. Chagua aina ya maudhui unayoipendelea na njia ya kuyatazama.
  2. Chagua na ufute maudhui unayoyataka.
    Unaweza kufuta faili ambazo zimeshirikiwa kutoka vifaa vingine.
  3. Chagua maudhui unayotaka kucheza. Unaweza tu kuchagua aina sawa ya maudhui na ile uliyochagua mwanzo.
  4. Unaweza kunakili maudhui na kuyabandika kwenye kifaa cha hifadhi cha USB.
    Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
  5. Fungua Tafutiza.
Baadhi ya maudhui huenda yasionyeshwe katika orodha ikiwa idadi ya maudhui yote inazidi 40,000.
Kicheza Picha
Kuchagua picha katika programu ya Picha & Video huendesha kicheza picha. Unaweza kutaza picha ulizohifadhi.

Kicheza pichaKicheza picha

  1. Hurejea kwenye orodha nzima ya maudhui.
  2. Unaweza kucheza muziki wa mandharinyuma kwa kufungulia kicheza muziki.
  3. Unaweza kukuza / kupunguza picha.
  4. Huanzisha onyesho la slaidi.
  5. Huzungusha picha.
  6. Picha za digrii 360 zinaweza kutazamwa katika dirii 360.
    Kutumia MCHEZO WA 360˚ VR kwa picha ya kawaida kunaweza kubadili umbo la picha.
    Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli pekee.
  7. Unaweza kuweka ukubwa wa picha au kubadilisha kasi na athari za uonyeshaji wa slaidi.
Faili za Picha Zinazotumika.
Faili za Picha Zinazotumika.
Umbizo la Faili Umbizo Ung’avu
jpeg, jpg, jpe JPEG Upeo wa chini : 64 × 64
Upeo wa juu
Aina ya Kawaida : 15360 (W) × 8640 (H)
Aina Endelevu : 1920 (W) × 1440 (H)
png PNG Upeo wa chini : 64 × 64
Upeo wa juu : 5760 (W) × 5760 (H)
bmp BMP Upeo wa chini : 64 × 64
Upeo wa juu : 1920 (W) × 1080 (H)
Kicheza Video
Kuchagua picha katika programu ya Picha & Video huendesha kicheza video. Unaweza kutazama picha ulizohifadhi.

Kicheza videoKicheza video

  1. Hurejea kwenye orodha nzima ya maudhui.
  2. Unaweza kuchagua maudhui mengine kwa kuonyesha orodha ya nyimbo wakati ukitazama video.
  3. Unaweza kudhibiti utendaji wa kawaida wa urudiaji video.
  4. Huzungusha video.
    Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli pekee.
  5. Video za digrii 360 zinaweza kutazamwa katika dirii 360.
    Kutumia MCHEZO WA 360˚ VR kwa video ya kawaida kunaweza kubadili umbo la picha.
    Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli pekee.
  6. Kwa kukuza kionyesho cha TV, unaweza kuangalia picha kwa kiwango kikubwa zaidi ya kiwango halisi.
    Kwa maelezo zaidi, angalia Manufaa ya TV Inayoweza Kuunganishwa kwenye Intaneti Kupanua Skrini ya TV katika Mwongozo wa Mtumiaji.
  7. Unaweza kuweka chaguo za ziada.
Kuweka Chaguo za Ziada

Chaguo kadhaa za kicheza videoChaguo kadhaa za kicheza video

  1. Unaweza kubadilisha mipangilio ya manukuu.
  2. Unaweza kuweka nyimbo za kusikilizwa tu.
  3. Unaweza kuweka utendaji wa endelea kutazama ili uendelee kutazama kutoka ulipoachia.
    Televisheni inpowashwa kwa kutumia Anza Haraka+, utendaji endelea kutazama huenda usiwezekane mara moja.
  4. Unaweza kuweka urudiaji wa usiokoma.
    Kama urudiaji wa kuendelea utawekwa, video inayofuta itachezwa kiotomatiki baada ya video iliyokuwa ikirudiwa kumalizika.
  5. Hurejea kwenye skrini ya utendaji wa kawaida.
Faili za Video Zinazotumika.
Kiwango cha juu cha kuhamisha data:
Manukuu ya kando yanayotumika
smi, srt, sub (MicroDVD, SubViewer 1.0/2.0), ass, ssa, txt (TMPlayer), psb (PowerDivX), dcs (DLP Cinema)
Umbizo la manukuu yanayotumika
Matroska (mkv) : Alpha ya Kituo Kidogo (SSA), Alpha ya Juu ya Kituo Kidogo (ASS), SRT
MP4 : Maandishi Yaliyowekewa Muda
Kodeki za video zinazotumika.
Urefushaji, Kodeki
Urefushaji Codec
asf
wmv
Video VC-1 Wasifu wa Hali ya Juu (isipokuwa kwa WMVA), VC-1 Wasifu Nyepesi na Kuu
Sauti WMA Standard (isipokuwar WMA v1 / WMA Speech)
avi Video Xvid (isipokuwa kwa pionti 3 za wapu GMC), H.264/AVC, Mwendo Jpeg, MPEG-4
Sauti MPEG-1 Layer I, II, MPEG-1 Layer III (MP3), Dolby Digital, LPCM, ADPCM, DTS
mp4
m4v
mov
Video H.264/AVC, MPEG-4, HEVC
Sauti Dolby Digital, Dolby Digital Plus, AAC, MPEG-1 Layer III (MP3), Dolby AC-4
3gp
3g2
Video H.264/AVC, MPEG-4
Sauti AAC, AMR-NB, AMR-WB
mkv Video MPEG-2, MPEG-4, H.264/AVC, VP8, VP9, HEVC
Sauti Dolby Digital, Dolby Digital Plus, AAC, PCM, DTS, MPEG-1 Layer I, II, MPEG-1 Layer III (MP3)
ts
trp
tp
mts
Video H.264/AVC, MPEG-2, HEVC
Sauti MPEG-1 Layer I, II, MPEG-1 Layer III (MP3), Dolby Digital, Dolby Digital Plus, AAC, PCM, Dolby AC-4
mpg
mpeg
dat
Video MPEG-1, MPEG-2
Sauti MPEG-1 Layer I, II, MPEG-1 Layer III (MP3)
vob Video MPEG-1, MPEG-2
Sauti Dolby Digital, MPEG-1 Layer I, II, DVD-LPCM
rm
rmvb
Video RV30, RV40
Sauti Realaudio6 (cook), AAC LC, HE-AAC
rm, rmvb : Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
Dolby AC-4 : Kipengee hiki kinapatikana katika baadhi ya modeli pekee.
Tahadhari katika Kutumia Kipengee cha Urudiaji Wimbo au Video
Baadhi ya manukuu yaliyoundwa na watumiaji huenda yasifanye kazi vyema.
Faili ya video pamoja na manukuu yake sharti ziwe kwenye kabrasha moja. Ili manukuu yaonyeshwe vyema, hakikisha kwamba faili ya video na faili ya manukuu zina jina moja.
Manukuu katika kifaa cha Hifadhi Iliyounganishwa kwenye Mtandao (NAS) huenda yasitumike kutegemea mtengezaji wa kifaa au modeli.
Mipasho ambayo inajumuisha Global Motion Compensation (GMC) na Quarterpel Motion Estimation (Qpel) haitumiki.
Video ya ULTRA HD (Modeli ya ULTRA HD pekee) : 3840 × 2160, 4096 × 2160
Ukubwa wa faili zinazoweza kuchezwa unaweza kutofautiana kutegemea hali za usimbaji.
Ni Window Media Audio V7 pekee na matoleo ya baadaye yanayotumika.
Wasifu mkuu wa AAC hautumiki.
Faili za video zilizoundwa na baadhi ya wasimbaji huenda zisichezwe.
Faili za video zilizo katika umbizo tofauti na zilizobainishwa huenda zisichezwe vyema.
Faili za video zilizohifadhiwa katika vifaa vya hifadhi vya USB ambazo hazitumii Mwendo wa Kasi huenda zisichezwe vyema.
Misimbo ya DTS inatumika tu kwa uchezaji wa faili za video za USB na HDMI.