Kushiriki Maudhui ni nini?
Kushiriki Maudhui hukwezesha kufurahia video, muziki na picha zilizohifadhiwa katika kompyuta yako.
Cheza maudhui kwa kutumia programu ya kushiriki iliyo kwenye kompyuta
Ikiwa una Windows 7 au toleo jipya zaidi kwenye kompyuta yako, unaweza kucheza video, muziki, video, picha nk. Kwenye TV yako bila kuhitaji kusakinisha programu nyingine.
  1. Unganisha TV na kompyuta yako kwenye mtandao mmoja. Kompyuta zilizo na Windows 7 au toleo jipya zaidi zinahitaji kuunganishwa kwenye mtandao.
  2. Bofya kulia kwenye faili ya muziki / video / picha unayotaka kucheza, kisha uchague modeli yako kwa kutumia kipangele cha “Play To” kilicho ndani ya Windows 7 au toleo jipya zaidi ili ucheze faili hii.
    Ili kucheza kwenye vifaa vingine kama vile simu yako ya mkononi, rejelea mwongozo mwafaka wa mtumiaji.
Hata pale mbapo televisheni au vifaa vingi vimeunganishwa, faili iliyochaguliwa itachezwa kupitia kifaa kimoja tu. Kiwango cha urudiaji video kinaweza kutofautiana kutegemea muunganisho wa mtandao.
Tumia Programu ya SmartShare ya kompyuta kucheza maudhui yaliyohifadhiwa kwenye kompyuta
Unaweza kutumia Programu ya SmartShare ya kompyuta kuunganisha muziki / video / picha zilizohifadhiwa kwenye kompyuta na mtandao wako wa nyumbani na uzicheze kwenye televisheni yako.
  1. Sanidi televisheni na kompyuta zilizosakinishwa kwa SmartShare katika mtandao mmoja.
    Huduma ya SmartShare inapatikana tu wakati televisheni na kompyuta ya seva zimeunganishwa kwa kielekezi kimoja.
  2. Pakua na usakinishe Programu ya kompyuta ya SmartShare kutoka kwa tovuti ya LG.
    Kabla ya kusakinisha, toka kwenye programu zote zinazoonyeshwa kwenye kompyuta, kama vile ngome au kinga-virusi.
  3. Fungua Programu ya SmartShare ya kompyuta na usanidi mipangilio ya kushiriki.
  4. Video na picha zilizoshirikiwa zitachezwa kutoka kwenye programu ya Picha & Video kwenye televisheni. Faili za muziki zilizoshirikiwa zitachezwa kutoka kwenye programu ya Muziki kwenye televisheni.
Seva inapaswa kuwa ikifanya kazi ili uweze kutazama faili iliyoshirikiwa kwenye televisheni.
Unaweza kuangalia maelezo ya tovuti katika MWANZOMWANZO KIUNGANISHI CHA KIFAA PC SHIRIKI MAUDHUI.
Kwa maelezo kuhusu namna ya kutumia programu ya SmartShare ya kompyuta, rejelea sehemu ya usaidizi kuhusu programu.
Maswala ambayo yanahitaji kuzingatiwa kwa makini wakati wa Kushiriki Maudhui
Angalia mipangilio yako ya mtandao kama chaguo la Kushiriki Maudhui halifanyi kazi vizuri.
Huenda isifanye kazi vizuri katika mtandao wa pasi waya. Inapendekezwa kwamba uunganishe na mtandao unaotumia nyaya.
Huenda isifanye kazi vizuri kutegemea mazingira ya mtandao.
Kama televisheni kadhaa zimeunganishwa kwenye kifaa kimoja, huenda maudhui yasichezwe vizuri kutegemea utendaji wa seva.
Ili kutazama video ya 1080p kupitia utendaji wa Kushiriki Maudhui, kielekezi ambacho hutumia masafa ya 5 GHz kinahitajika. Kama kielekezi cha 2.4 GHz kitatumiwa, huenda video isicheze vizuri.
Huenda utendaji wa Kushiriki Maudhui hautumiki kwa kielekezi kisichotumia maonyesho mengi. Kwa maelezo zaidi, rejelea mwongozo wa mtumiaji ulikuja na kielekezi au uwasiliane na mtengenezaji kielekezi.
Manukuu yanatumika tu katika baadhi ya vifaa vilivyounganishwa.
Programu ya SmartShare ya kompyuta inapendekezwa kwa kusoma manukuu.
Faili ya manukuu mapya inapoongezwa, lemaza folda iliyoshirikiwa halafu uiwezeshe tena.
Faili za DRM zilizo katika kifaa kilichounganishwa hazitacheza.
Hata kwa umbizo la faili linalotumika kwenye televisheni, umbizo la faili lialotumika linaweza kutofautiana kutegemea mazingira ya kifaa kilichounganishwa.
Kuna kabrasha au faili nyingi sana katika kabrasha, huenda isifanye kazi vizuri.
Maelezo yaliyo kwenye faili iliyoletwa kutoka kwenye kifaa kilichounganishwa huenda yasionyeshwe kwa njia sahihi.
Kutegemea usimbaji, huenda baadhi ya mipasho isicheze katika modi ya Kushiriki Mudhui.