Kushiriki Maudhui kwa Kutumia Simu Mahiri
Kushiriki Maudhui hukuwezesha kufurahia video, muziki na picha zilizohifadhiwa katika simu mahiri yako ambayo umenganishwa katika mtandao sawa.
Kuunganisha kwenye Simu Mahiri Ukitumia Televisheni Yako
  1. Bonyeza kitufe cha MWANZOMWANZO katika kidhibiti cha mbali.
  2. Unaweza kuanzisha programu ya KIUNGANISHI CHA KIFAA.
  3. Chagua Simu mahiri.
  4. Fuata maagizo katika KIUNGANISHI CHA KIFAA.

Kiunganisha vifaaKiunganisha vifaa

Maswala ambayo yanahitaji kuzingatiwa kwa makini wakati wa Kushiriki Maudhui
Angalia mipangilio yako ya mtandao kama chaguo la Kushiriki Maudhui halifanyi kazi vizuri.
Huenda isifanye kazi vizuri katika mtandao wa pasi waya. Inapendekezwa kwamba uunganishe na mtandao unaotumia nyaya.
Huenda isifanye kazi vizuri kutegemea mazingira ya mtandao.
Kama televisheni kadhaa zimeunganishwa kwenye kifaa kimoja, huenda maudhui yasichezwe vizuri kutegemea utendaji wa seva.
Ili kutazama video ya 1080p kupitia utendaji wa Kushiriki Maudhui, kielekezi ambacho hutumia masafa ya 5 GHz kinahitajika. Kama kielekezi cha 2.4 GHz kitatumiwa, huenda video isicheze vizuri.
Manukuu yanatumika tu katika baadhi ya vifaa vilivyounganishwa.
Faili ya manukuu mapya inapoongezwa, lemaza folda iliyoshirikiwa halafu uiwezeshe tena.
Faili za DRM zilizo katika kifaa kilichounganishwa hazitacheza.
Hata kwa umbizo la faili linalotumika kwenye televisheni, umbizo la faili lialotumika linaweza kutofautiana kutegemea mazingira ya kifaa kilichounganishwa.
Kuna kabrasha au faili nyingi sana katika kabrasha, huenda isifanye kazi vizuri.
Maelezo yaliyo kwenye faili iliyoletwa kutoka kwenye kifaa kilichounganishwa huenda yasionyeshwe kwa njia sahihi.
Kutegemea usimbaji, huenda baadhi ya mipasho isicheze katika modi ya Kushiriki Mudhui.