Kuunganisha USB
Unganisha kifaa cha hifadhi cha USB (hifadhi ya USB HDD, USB) kwenye lango la USB kwenye TV ufurahie maudhui yaliyo kwenye faili zilizohifadhiwa katika kifaa cha hifadhi cha USB kilicho kwenye TV yako.
Vidokezo kuhusu namna ya kutumia Vifaa vya hifadhi vya USB
Kifaa cha hifadhi cha USB ambacho kimejengewa ndani programu ya kutambua kiotomatiki au kinachotumia dereva zake binafsi huenda kisitambuliwe.
Baadhi ya vifaa vya hifadhi vya USB huenda havitumiki au huenda havifanyi kazi vizuri.
Kama utatumia kebo ya USB, huenda kifaa cha hifadhi cha USB kisitambuliwe au kufanya kazi vizuri.
Tafadhali tumia vifaa vya hifadhi vya USB vilivyoumbizwa kwa mfumo wa faili wa FAT32 au NTFS ambao hutolewa na Windowa OS.
Inapendekezwa kwamba utumie hifadhi ya USB,HDD ya kando yenye volteji ya 5V au chini na moto wa 500 mA au chini.
Inapendekezwa utumie kitovu cha USB au USB HDD ikiwa na chanzo cha nishati. (Ikiwa nishati inayotumika haitoshi, kifaa cha hifadhi ya USB huenda kisitambulike vizuri.)
Inapendekezwa utumie hifadhi ya USB ya GB 32 au chini ya hizi au USB HDD ya TB 2 au chini ya hizi.
Kama USB HDD iliyo na utendaji wa kuhifadhi chaji haifanyi kazi, zima hifadhi kuu kisha uiwashe ili ifanye kazi vizuri. Kwa maelezo zaidi kuhusu USB HDD, angalia mwongozo wa matumizi.
Data katika kifaa cha hifadhi cha USB inaweza kuharibiwa. Inapendekezwa kwamba uweke nakala rudufu ya faili zozote muhimu. Watumiaji watawajibikia udhibiti wa data. Mtengenezaji vifaa hatalipia gharama yoyote.
Chagua USB iliyounganishwa kutoka Maingizo halafu uchague kitufe cha Ondoa ili kuondoa kifaa cha USB.
Ukitoa kifaa cha hifadhi ha USB bila kuchagua Ondoa, hitilafu inaweza kutokea kwenye telvisheni au kifaa cha hifadhi.
Unaweza kufungua Maingizo kwa kuchagua
Maingizo Yote.
Pia unaweza kwenda kwenye hifadhi ya USB katika
halafu ubonyeze Ondoa.
Unaweza kufungua Maingizo kwa kuchagua
Maingizo Yote.
Pia unaweza kwenda kwenye hifadhi ya USB katika
halafu ubonyeze Ondoa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu njia nyingine za kuunganisha enda kwa
KIUNGANISHI CHA KIFAA.
KIUNGANISHI CHA KIFAA.
Chagua USB iliyounganishwa kutoka Maingizo halafu uchague kitufe cha Umbiza kuumbiza kifaa cha USB.
Baada ya kuumbiza, data yote iliyo katika kifaa cha hifadhi cha USB itafutwa na iumbizwe kama mfumo wa faili wa NTFS au FAT32.
Unapounganisha kifaa cha hifadhi cha USB faili / kabrasha bila mpangilio wowote inaweza kuundwa ili kuipa Televisheni Mahiri huduma za kama vile kuhifadhi na kurejesha vijipicha.