Kuona skrini ya Simu ya Mkononi kwenye Televisheni
- Wezesha hali ya Miracast kwenye simu yako ya mkononi.
- Televisheni yako itaonyeshwa kwenye orodha ya vifaa vinavyopatikana.
- Chagua runinga yako kisha uombe muunganisho.
- Chagua Ndiyo katika kidirisha cha idhini kitakachotokea.
- Baada ya muunganisho kupatikana, televisheni itaonyesha skrini ya kifaa kilichounganishwa.
- Hubadilisha nafasi ya skrini ya kifaa cha mkononi.
- Hubadilisha sauti kutoka kwenye TV hadi kifaa cha mkononi.
- Huonyesha skrini ya kifaa cha mkononi katika hali ya skrini nzima.
- Tok kwenye Screen Share.
Kutumia Hali ya Kufunika kunaweza kukosa kutumika vizuri kulingana na programu au video iliyofunguliwa.
Kwa muunganisho wa kutegemewa, kila mara, hakikisha kifaa kilichounganishwa kwenye televisheni yako kimesasishwa hadi toleo la hivi karibuni la OS.
Huenda kifaa ambacho si cha LGE kisiunganishwe hata kama kimetambulika.
Unganisha kifaa na kielekezi cha 5 GHz kwa sababu utendaji unaweza kuathiriwa na mazingira kilipo kifaa chako kisichotumia nyaya.
Kiwango cha kutumika kinaweza kutofautiana kutegemea mazingira ya mtumiaji.
Hutofautiana miongoni mwa vifaa. Unapojaribu kuunganisha kwenye kifaa, rejelea mwongozo wa matumizi kwa maelezo zaidi.
Muunganisho ukikosekana mara kwa mara, zima televisheni na kifaa unachojaribu kuunganisha. Kisha ziwashe na ujaribu tena.