Hitilafu za Akaunti ya LG
Kama utakumbana na mojawapo ya matatizo yaliyoorodheshwa hapa chini wakati unapotumia bidhaa, tafadhali angalia vitu vifuatavyo. Huenda bidhaa haina tatizo lolote.
Tayari nimejisajili kwenye televisheni. Lazima nijisajili tena katika tovuti (www.lgappstv.com)?
Kama umeshajisajili kwenye televisheni yako, hufai kujisajili tena kwenye tovuti.
Unaweza kuingia katika tovuti kwa kutumia kitambulisho na nywila sawa kisha uingize maelezo ya ziada ili kukamilisha mchakato wa uthibitishaji wa barua pepe.
Je, inawezekana watu wa familia moja kutumia vitambulisho tofauti kwa televisheni moja?
Unaweza kusajili vitambulisho kadhaa kwa kila skrini.
Nimesahau kitambulisho / nywila langu. Nitafanya nini?
Unaweza kuanzilisha nywila kupitia barua pepe unapochagua UMESAHAU NYWILA? Katika skrini ya kujisajili.
Kama ulijisajili kwenye televisheni, unaweza kupata kitambulisho / nywila lako katika tovuti (www.lgappstv.com).
Katika baadhi ya nchi, ufikiaji wa tovuti (www.lgappstv.com) unaweza kuwa umezuiliwa.