Hitilafu za Kuunganisha kwenye Mtandao
Kama utakumbana na mojawapo ya matatizo yaliyoorodheshwa hapa chini wakati unapotumia bidhaa, tafadhali angalia vitu vifuatavyo. Huenda bidhaa haina tatizo lolote.
Unaweza kukagua hali ya mtandao jinsi inavyoonyeshwa hapa chini.
-
Mtandao
Muunganisho Ulio na Waya (Ethaneti)
-
Mtandao
Muunganisho wa Wi-Fi
Mipangilio ya kiwango cha juu ya Wi-Fi
-
X ikitokea karibu na televisheni -
Angalia televisheni au AP (Kielekezi).
- Angalia hali ya muunganisho ya TV, AP(Kielekezi) na Modemu Inayotumia Kebo.
- Washa na uzime katika mpangilio ufuatao;
1. Modemu inayotumia kebo, subiri Modemu inayotumia Kebo iwekwe upya.
2. AP (Kielekezi), subiri AP (kielekezi) kiwekwe upya.
3. Televisheni- Kama unatumia muunganisho wa pasi waya, badilisha SSID (Jina la Mtandao) na kituo cha AP (Kielekezi) cha pasi waya.
- Kama unatumia IP isiyosonga, ingiza IP moja kwa moja.
- Wasiliana na mtoa huduma za Intaneti au kampuni za AP (Kielekezi).
-
X ikitokea karibu na Gateway - Angalia AP (kielekezi) au ushauriane na mtoa huduma wako wa Intaneti.
- Toa kebo ya stima ya AP (Kielekezi) Modemu Inayotumia kebo kisha usubiri sekunde 10. Weka nishati tena.
- Anzilisha (Weka upya) kwenye AP (Kielekezi) au Modemu Inayotumia kebo.
- Wasiliana na mtoa huduma za Intaneti au kampuni za AP (Kielekezi).
- Angalia AP (kielekezi) kwenye tovuti ya mtengenezaji wa bidhaa ili kuhakikisha kuwa kielekezi chako kina toleo la hivi karibuni la kinga-virusi iliyasakinishwa.
-
X ikitokea karibu na DNS - Angalia AP (kielekezi) au ushauriane na mtoa huduma wako wa Intaneti.
- Toa kebo ya stima ya AP (Kielekezi) Modemu Inayotumia kebo kisha usubiri sekunde 10. Weka nishati tena.
- Anzilisha (Weka upya) kwenye AP (Kielekezi) au Modemu Inayotumia kebo.
- Hakikisha kuwa anwani ya MAC ya kielekezi cha TV / AP imesajiliwa na mtoa huduma wako wa Intaneti. (Anwani ya MAC iliyoonyeshwa kwenye upau wa dirisha la hali ya mtandao inapaswa kusajiliwa na mtoa huduma wako wa Intaneti.)